Oktoba hii Safina ya Ladha ya Hamasisha Bidhaa Mpya

28 Aug 2014 | Swahili

Mwaka huu mkusanyiko wa Salone del Gusto na Terra Madre utatenga nafasi ili kuzingatia kwa undani mradi wa kimataifa wa Safina ya Bidhaa za Ladha. Mradi huu wa kimataifa uliundwa ili kuhifadhi utofauti wa mimea, ambayo inaendelea kupotea kwa kukusanya na kuhifadhi vifaa msingi vya kilimo endelevu ili  kuhifadhi mila na desturi zetu na kuepuka njia ambazo makampuni hutumia ili kubadilisha mazao ya vyakula  vya kitamaduni. Kilimo endelevu cha jumuisha aina za ukulima na uzalishaji uliotumiwa hapo awali, pamoja na tamaduni tulizorithi za kupanda matunda, mboga, kuzalisha wanyama, kutengeneza jibini, kuoka mikate na pia jinsi ya kuhifadhi nyama na tamutamu; zilizopotea na kusahauliwa kwa miaka kadhaa na sekta ya chakula ambayo imekuwa ikitumia kiasi kidogo cha vyakula vinavyopatikana, jambo hili huharibu mazingara na hupunguza matumizi ya bidhaa tofauti na hivyo kutunyima uwezo wetu wakuchagua.

Kwenye mradi huu wa kimataifa Slow Food hutoa mwito kwa kila mtu kusaidia kulinda na kuunga mkono wakulima na wazalishaji wanaoendeleza kilimo endelevu na tamaduni zao. Safina ya Bidhaa ni hatua ya kuanza kutilia mkazo dhamani ya bidhaa ambazo ziko katika njia ya kusahaulika, hii ni sababu kuu ambayo katika mkusanyiko wa Salone del Gusto na Terra Madre kutakuwa na mfululizo wa warsha na mikutano itakayowezesha wahudhuriaji kufaidika na maelezo zaidi na kuwapa fursa ya kuonja bidhaa za Safina kutoka duniani kote.

Safina ya Bidhaa za Ladha katika maonyesho ya Terra Madre na Salone del Gusto:

Mamia ya bidhaa zilizo katika Safina zitakuwa kwenye maonyesho katika eneo la Oval, ambapo soko la kimataifa litapatikana. Hili ni eneo la mita 600 mraba lililotengwa kwa ajili ya kilimo endelevu. Vyakula bichi ambavyo vinaweza kuharibika vitatengewa nafasi kwenye pande za jumba hili, mifugo itakuwa inawakilishwa kwa njia ya picha na makala ya filamu. Pia Slow Food inakaribisha wageni wote kuleta bidhaa ambazo wanaamini kuwa lazima zilindwe kwa ajili ya vizazi vijavyo kwenye Safina ya Ladha. Hii itakuwa fursa nzuri ya kukutana na wakulima na wafugaji kutoka pembe zote za dunia ambao wataonyesha bidhaa zao. Mpiga picha mashuhuri Oliviero Toscani kutoka Italia ambaye kwa muda ameshirikiana na Slow Food, atakuwepo ilikuonyesha kazi yake na picha alizopiga za Safina ya Ladha.

Safina ya Ladha pia itatiliwa mkazo katika tahadhari ya mikutano zifuatazo:

Safina ya linda bidhaa za ladha Jumamosi, Oktoba 25, 2014

Safina ya Ladha katika Iceland Alhamisi, Oktoba 23, 2014

Safina ya Ladha katika bara la Asia  Alhamisi, Oktoba  23, 2014

Safina ya Ladha katika bara la Africa Jumamosi Oktoba, 25, 2014

Safina ya Ladha katika America Latina Jumamosi, Oktoba 25, 2014

Safina ya ladha katika bara la Eurasia Jumatatu, Oktoba 27, 2014

Safina ya Ladha katika America ya kusini  Jumatatu, Oktoba 27, 2014

Wakati wa mfululizo wa Warsha za ladhaa katika Salone del Gusto, wahudhuriaji watapewa fursa ya kujifunza na kuonja bidhaa mbalimbali kutoka duniani kote. Kwa mfano:

Wachinja nguruwe wa kitamaduni jumamosi, Oktoba  27, 2014

Mtandao wa kimataifa wa wauzaji jibini  Jumatatu, Oktoba 27, 2014

Mvinyo wa pikwa huko Scandinavia Ijumaa, Oktoba 24, 2014

Divai na Maeneo: Historia ya Mabadiliko Alhamisi, Oktoba 23, 2014

Abracadabra… Amphora! Ijumaa, Oktoba 24, 2014

Fursa ya kujua na kuonja chai ya Pu’er  Jumatatu, Oktoba 27, 2014

Historia na kahawa ya kwanza nchini Uhabeshi. Alhamisi, Oktoba 23, 2014

Kuomba kibali cha SDG/TM 2014 ,tembelea  http://www.salonedelgusto.com/press/pre-accreditation/

Kwa habari zaidi wasiliana nasi kupitia:

℅ Slow Food Paola Nano, +39 329 8321285 [email protected]

           c/o Regione Piemonte: Tel. +39 011 4322549 [email protected]

           c/o Comune di Torino: Tel. +39 011 4423605 [email protected]

Iliyoandaliwa na Slow Food, mkoa wa Piedmont na mji wa Turin, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Chakula na sera za misitu, tukio la kimataifa ‘Salone del Gusto’ tukio linarejea tena Turin, Italia, sasa ndio mwaka wake wa 10. Kujitolea katika ulimwengu wa chakula, Salone del Gusto mara nyingine zaidi inajumuika katika tukio moja kwa mkutano wa kimataifa wa ‘Terra Madre’, mtandao wa wazalishaji wadogo wadogo kutoka duniani kote. Salone del Gusto na Terra Madre 2014 zitafanyika kuanzia Oktoba 23-27 katika Turin’s trade fair Lingotto Fiere. Itakuwa kuona uwepo wa zaidi ya 1,000 washiriki kutoka nchi 130.

Change the world through food

Learn how you can restore ecosystems, communities and your own health with our RegenerAction Toolkit.

Please enable JavaScript in your browser to complete this form.
Full name
Privacy Policy
Newsletter